Boga ni tunda ambalo watu wengi wanalipuuzia, ni tunda lenye virutubisho vingi na lina faida nyingi kiafya tunda hili i chanzo kizuri cha virutubisho aina ya BETA CAROTENE amabvyo vinafanya boga kuwa rangi ya njano lakini pia kunavirutubisho kama Potassium, vitamin C vitamin E, na madini ya chuma kwa wingi.

Zifuatazo ni faida za Boga katika mwili wa binadamu..

Boga linakiwango kikubwa cha Potassium ambacho husaidia kupunguza kiwango cha soddium mwilini ambayo hupelekea kuongezeka kwa shinikizo la damu, hivyo bongo ni mojawapo ya vyakula muhimu kwa mtu mwenye presha ya kupanda

Utafiti uliofanywa na kitengo cha lishe cha Chuo kikuu cha Havard USAunaonesha kuwa kula vyakula vyenye beta calotene inasaidia kuzuia saratani ya dume.

Boga lina Vitamin C, Vitamin E, virutubisho hivi pamoja na Beta calotene husaidia kuimarisha afya ya macho,na kuzuia tatizo la kutoona vizuri wakati wa uzee.

Madini ya chuma ambayo yanapatikana katika boga ni muhimu kwa wanawake ambao wapo katika umri wa kuzaa kwani yanasaidia kuchochea uzazi pia vitamin A inayotokana na beta calotene ni muhimu kwa afya ya mama mjamzito anayenyosha.

Serikali yatoa tamako zuio la kuingia Uingereza
Mwili wa Martha kuagwa leo Bungeni