Wataalamu wanaelezea tikiti maji kama tunda ambalo ni muhimu sana kwa afya ya binadamu, kwasababu ina madini ya hali ya juu ya ikiwa ni pamoja ya Vitamini, Midini, Vizuia oksidi na Mafuta.

Tikiti maji lina asilimia 92 ya maji, ikimaanisha kuwa wale wanaotumia tunda hilo hawana hofu ya kukabiliwa na ukosefu wa maji mwilini, anasema mtaalamu wa masuala ya lishe bora Maijidda Badamasi Burji.

Imebainika kuwa mbegu za matikiti huimarisha afya ya uzazi ya wanandoa, hasa kina baba, na hivyo kuwa na fursa kubwa ya kuongeza furaha baina ya wapendano.

Imethibitika kuwa kuwa mbegu hizo zina asilimia 74 ya madini ya manganizi, asilimia 57 ya phosphorosu, asilimia 48 ya magnezium, asilimia 48 ya shaba, asilimia 23 ya zinc, asilimia 20 ya protini na asilimia 16 ya chuma, vyote vikiwa ni virutubisho muhimu mwilini mwa kila mwanadamu, wakiwamo wanandoa wenye nia ya kuongeza furaha katika mahusiano yao ya kiunyumba.

Ulaji wa tikitimaji husaidia kupunguza uwezekano wa kukabiliwa na shinikizo la damu lakini pia kusaidia mmeng’enyo wa chakula na faida nyingine kuongeza mafuta yasiyokuwa na lehemu na kuipa afya mishipa ya fahamu na sita, ni kuimarisha afya ya ngozi.

Mbegu za matikiti zimejaaliwa kuwa na viinilishe vingi sana, kuna protini, vitamin na madini mengi yakiwamo ya chuma, zinc, shaba, potassium, magnesium, phosphorous, sodium na manganese.

Ingawa bado kuna tafiti mbalimbali zinaendelea kufanyika hasa nchini Marekani, lakini utafiti wa awali umeonyesha kuwa mbegu za tikiti zina uwezo wa kuwasaidia kwa kiasi kikubwa watu wenye kisukari na pia kuimarisha mifumo ya figo.

Shirika la Afya Duniani (WHO) limependekeza ulaji wa tunda hilo kwa sababu humsaidia mtu kupata vitu vingi muhimu kwa wakati mmoja.

Tozo za simu, miamala bado moto
Rais Samia afanya uteuzi