Uwanja wa Sheikh Amri Abeid umetajwa kuwa mwenyeji wa mchezo wa Fainali Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ msimu huu 2021/22, baada ya kutajwa kwa viwanja vitakavyotumika kwa michezo ya Nusu Fainali ya michuano hiyo.

Sheikh Amri Abeid ambao ni Uwanja mkongwe katika ardhi ya Tanzania, pia utakua mwenyeji wa mchezo wa Nusu Fainali ya pili ya ASFC, ambao utashuhudia Azam FC ya Dar es salaam ikicheza dhidi ya Coastal Union ya Tanga, Jumapili (Mei 29).

Uwanja CCM Kirumba uliopo jijini Mwanza utakua mwenyeji wa Nusu Fainali ya kwanza ya ASFC, ambao utashuhudia miamba ya Soka la Bongo Simba SC na Young Africans ikipepetana kusaka nafasi moja ya kutinga Fainali, sikui ya Jumamosi (Mei 28).

Kwa mujibu wa TFF, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid umethibitishwa kuwa mwenyeji wa mchezo wa Fainali kupitia kurasa za mitandao ya kijamii za Shirikisho hilo leo Jumatatu (Mei 16), ambapo mchezo huo utapigwa Julai Mbili.

Hii itakua mara ya pili kwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kuwa mwenyeji wa mchezo huo, baada ya kupewa hadhi hiyo misimu mitatu iliopita ambapo Mtibwa Sugar ilitwaa ubingwa dhidi ya Singida United.

Msimu uliiopita 2020/21 mchezo wa Fainali uliozikutanisha Simba SC na Young Africans, ulipigwa Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma, huku michezo ya Nusu Fainali ikichezwa katika viwanja wa Alli Hassan Mwinyi na Majimaji mkoani Ruvuma.  

Habari kuu kwenye magazeti ya Leo Mei 17, 2022
'Huddah The Boss' aangukia kwa Mwanariadha Omanyala