Faiza Ally ameeleza faida anazopata kutokana na mtandao wa Instagram ambao amedai mbali na kumpa umaarufu na kushambuliwa kwa picha ‘tata’ anazoweka,  umemuwezesha kumudu gharama za maisha.

Faiza ambaye ni mzazi mwenza wa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph ‘Sugu’ Mbilinyi, amefunguka jana wakati wa maadhimisho ya siku ya mama duniani, alipokuwa Mlimani City jijini Dar es Salaam alipokwenda kuangalia uzinduzi wa filamu mpya ya ‘Mama ni Mungu wa Dunia’ ya Aunt Ezekiel.

Faiza Ally na Mwanaye

Mwigizaji huyo ambaye amesema kuwa anajivunia kuwa mama, amesema hutumia mtandao huo kuweka matangazo na kufanya biashara zinazompa kipato ambacho kimemfanya kuwa mama anayemhudumia vizuri mwanaye.

Katika hatua nyingine, Faiza alisema kuwa kutokana na uzoefu wake kama mama, anawashauri wanawake wanaotaka kupata mtoto wasipate mtoto kama hawajajiandaa kumtunza kwani maisha yamebadilika. Hivyo, kwake kuweza kutunza mtoto au watoto akiwa peke yake kunamfanya ajivunie.

“Unajua unapokuwa mama, kuwa mama ni kama cheo. Kwahiyo unapofanya majukumu yako vizuri unajivunia, kwahiyo ‘I am proud of myself,” alisema na kuongeza kuwa hana mpango wa kuzaa mtoto mwingine hadi atakapokuwa na ukwasi wa kutosha.

Mrembo huyo alidai kuwa ingawa anapenda kufunga ndoa, anayafurahia pia maisha yake ya hivi sasa kwakuwa haamini kama maisha ya ndoa ndiyo maisha pekee bora.

 

 

 

 

Man United yawapiku Man City, Barca, Madrid
Haya ndio magonjwa yanayotibika kwa ''massage''

Comments

comments