Msanii maarufu wa muziki wa Rhumba kutoka DRC Congo mwenye makazi yake nchini Ufaransa Fally Ipupa N’simba amefunguka kwa undani namna anavyoifahamu tasnia ya Muziki wa bongo fleva na wasanii wake, huku akiwataja wasanii kadhaa wa Tanzania ambao ni miongoni mwa anaowafuatilia na kufahamu kwa undani zaidi kazi zao.

Fally Ipupa amemtaja msanii Diamond Platnumz na namna walivyoshirikiana kuutengeneza wimbo #Inama ikiwa ni pamoja na kugusia uhusiano wake na msanii Ali Kiba tangu walipokutana nchini Marekani kwenye utengenezaji wa wimbo maarufu #HandsAcrossTheWorld ulisimamiwa na msanii maarufu wa Marekani Robert Kelly maarufu R-Kelly

Fally Ipupa ameyazungumza hayo wakati akiongea na wana habari kuelekea show yake itakayofanyika katika ukumbi wa mlimani city, jumamosi  Tarehe 9 oktoba mwaka 2021, huku akiahidi kuzikonga nyoyo za mashabiki wake watakaojitokeza.

Waziri Gwajima awataka wananchi kuwa makini
Watalii 270 wawasili nchini