Familia ya Akwilina Akwiline, ambaye alifariki dunia Februari 16, 2018 imekabidhi bajeti ya mazishi ya binti yao kwa Serikali kiasi cha shilingi milioni 80.

Msemaji wa familia, Festo Kavishe amekabidhi bajeti hiyo leo, Jumanne Februari 20, 2018 kwa katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk. Leonard Akwipalo na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisali Makori .

Amesema ”Hayo ndiyo makubaliano ya familia, tumewakabidhi wataenda na kujadiliana kisha tutakutana nao leo jioni, kisha watatueleza ya kwao pia, tunachohitaji ndugu yetu apumzike kwa amani” amesema Kavishe.

Marehemu Akwilina amefikwa na mauti akiwa kwenye daladala baada ya kupigwa risasi ya kichwa, wakati wafuasi wa Chadema  wakiandamana kwenda kwa Mkurugezni wa Uchaguzi Wilaya ya Kinondoni kudai viapo vya wakala wao.

Marehemu Akwilina anatarajiwa kuagwa Alhamisi wiki hii katika viwanja vya NIT na kusafirishwa Rombo mkoani Kilimanjaro Ijumaa hii.

Mungu aipumzishe roho ya marehemu Akwilina mahali pema peponi, Salamu za pole ziwafikie ndugu jamaa na marafiki.

 

Hofu yatanda kwa waandishi wa habari kukamatwa kiholela
TRA yatoa matokeo ya uchunguzi uliofanywa kwa Askofu Kakobe, na kubaini haya