Baraza la mji wa Minneapolis nchini Marekani limeidhinisha makubaliano ya kuilipa familia ya George Floyd kiasi cha dola milioni 27.

Malipo hayo yanakuja ikiwa ni karibu mwaka mmoja tangu Mmarekani huyo Mweusi alipouwawa kutokana na hujuma za polisi.

Tangazo hilo limetolewa na Meya wa mji huo, Jacob Frey, katika mkutano na waandishi habari uliohudhuriwa pia na ndugu wa Floyd pamoja na wanasheria wa familia yake.

Hicho ni kiasi kikubwa zaidi cha fedha kuwahi kulipwa kwa familia za wahanga wa matendo ya jinai yanayofanywa na polisi na malipo hayo yanaondoa uwezekano wa familia ya Floyd kufungua kesi mahakamani.

Floyd alifariki dunia Mei, mwaka jana baada ya polisi mmoja mzungu kumkandamiza kwa goti shingoni kwa zaidi ya dakika nane katika tukio lililorikodiwa na mpita njia.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Machi 14, 2021
Miradi 281 ya maji kuzinduliwa