Baba mzazi wa Mwinyi Haji Ngwali (Bagawai) mchezaji wa Yanga na Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) amepania kulifungulia kesi gazeti la michezo la Bingwa baada ya kuandika habari ya iliokuwa ikumzungumzia mtoto wake kuwa ni mla unga (Teja).

Gazeti hilo liliandika taarifa hiyo ndefu siku ya Jumamosi ya April 30, mwaka huu ambapo kichwa cha habari kilikuwa kimeandikwa “ SIRI NZITO YAFICHUKA YANGA”, NYOTA ALIYEMKUNA MAHREZ WA LEICESTER NI TEJA WA KUTUPWA, APIGWA CHINI”.

IMG-20160502-WA0014

Taarifa hiyo ambayo imeandikwa na Muandishi Hussein Omar ambapo baba wa mchezaji huyo amesema msimamo wao ni kwenda Mahakamani kulifungulia kesi Gazeti hilo ili waandishi wa habari wapate funzo wanapoandika habari ziwe za uhakika na usahihi.

“ Nikiwa baba mzazi wa Mwinyi Haji Ngwali nasikitishwa kwa kitendo walichofanya Gazeti la Bingwa la tarehe 30/04/2016 kwa kuandikwa kuwa mtoto wangu ni Teja la kutupwa, hivyo kwa kitendo hicho imelichafua jina la mtoto wangu na familia yetu, kwa hivyo tumeamua kama familia msimamo wetu ni kufungua madai Mahakamani kwasababu baadhi ya waandishi wa habari wanakuwa hawapo sahihi kuandika habari zao”. Alisema mzee Haji.

Kanisa Katoliki lachomwa moto
Mahakama yamfunga mkuu wa chuo cha Uhasibu Arusha (IAA)