Familia ya Marehemu Suguta Marwa Suguta aliyeuawa kwa kuchomwa kisu na polisi imetoa msimamo mzito kuwa haitamzika ndugu yao hadi serikali itakapoweka ukweli wa tukio la kuuwawa kwa ndugu yao.

Uamuzi huo umefikiwa baada ya kikao cha familia kilichokutana jana katika Kijiji cha Sirari, wilayani Tarime mkoani Mara.

Mbunge wa Tarime, John Heche amesema kuwa licha ya kutoa taarifa rasmi kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba kuhusu mauaji ya ndugu yao kwani mpaka sasa hawajapata taarifa yeyote hata ya pole kutoka kwa Waziri huyo.

Heche ambaye ni msemaji wa familia amesema familia haijafikiria kuuzika mwili huo hadi ukweli utakapojulikana.

‘’Familia haitakuwa tayari kumzika Suguta hadi pale ambapo haki itatendeka kwani ni dhahiri linaviashirikia vya makusudi’’ amesema Heche.

Aidha Heche ameongezea kuwa uchunguzi wa daktari unaonesha kuwa marehemu Suguta alichomwa Kisu mgongoni kisu hiko kikaingia mpaka kwenye mapafu na moyo.

Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Henry Mwaibambe amesema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea kufanyika na tayari wanamshikilia askari aliyehusika na mauaji hayo.

Trump atishia kuifunga tena Serikali kuu ya Marekani
Sijui kama tutakutana tena na Mourinho- Arsene Wenger