Linaweza likawa ni jambo la ajabu na kustaajabisha hasa kwa familia ya Gwenny Blanckaert na Marino Vaneeno ambapo wamekuwa na utamaduni wa kipekee linapokuja suala la kuwapa majina watoto wao hutumia herufi zinazofana.

Aidha familia hiyo yenye jumla ya watoto 11 wa kike 7 na wa kiume 4 imekuwa ikitumia herufi 4 zinazofanana katika kuwapa majina watoto wao wote 11 ambapo herufi hizo ni A , X ,E na L.

Mtoto wa kwanza katika familia hiyo ni Alex ana miaka 13, akifuatiwa na Axel ( 12), Xela (11), Lexa ( 10), Xael (9), Xeal (8), Exla (5), Leax( 4), Xale (2), Elax (1), na Alxe ambaye ana miezi 6.

Hivi karibuni wazazi hao wanatarajia kupata mtoto wao wa mwisho wa kiume mwezi Aprili mwaka 2022 ambaye atakamilisha idadi ya wototo 12.

Waliovujisha mitihani kuchukuliwa hatua- Dkt Gwajima
Masau Bwire: Simba tulieni, msitetereke