Msemaji wa familia ya Lissu, wakili Alute Mughwai, amelitaka Bunge kutoa fedha za matibabu ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tudu Lissu, ambaye amelazwa katika hospitali ya Chuo Kikuu cha Luvein Ubelgiji.

Ambapo amesema kuwa yapata miezi mitano sasa Lisuu hajapata stahiki zake za matibabu kama mbunge.

“Tumemaliza miezi mitano tangu kutokea kwa tukio la kushambuliwa kwa Lissu na Bunge kama taasisi limeshindwa kutoa fedha za matibabu kwa mwenzao,” ame s sema Mughwai.

Ameongezea “Sasa Lissu atalaumiwaje? Akilia Mungu wangu mbona umeniacha, Bunge langu mbona limeniacha… au wanataka afukuzwe hapo hospitalini kwa kukosa fedha za matibabu?.

“Waheshimiwa hawa wanataka mwenzao kuwa kilema au kupoteza maisha? Cha msingi wanapaswa kutoa haki za msingi ambazo sisi tumeona zinacheleweshwa kwa makusudi.”

Kwa mujibu wa Bunge ambalo liliweka wazi kuhusu fedha za matibabu ya Lisu na kudai kuwa Lissu alifuata matibabu nje ya nchi kinyume na utaratibu wa bima ya afya ya wabunge, hivyo imekuwa kikwazo cha kuhudumiwa kwake.

Lissu (49) alipigwa risasi tano na watu wasiojulikana akiwa kwenye gari nyumbani kwake Area D mjini Dodoma Septemba 7, mwaka jana. Jumla ya risasi 32 zilirushwa na watu hao kwa mujibu wa taarifa za Bunge.

Akizungumzia afya ya Lissu, Mughwai amesema kwa sasa anaendelea vizuri na mazoezi ya viungo, ili kuimarisha afya yake.

Wafahamu viongozi wa Afrika waliowahi kujiapisha
LIVE: JPM akizindua Hati ya kusafiria ya Kielektroniki