Familia ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini, Marehemu Philemon Ndesamburo imekanusha kuwepo mgogoro kati yake na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuhusu rambirambi.

Aidha, familia hiyo imekanusha kuwa rambirambi zilizochangwa nje na ndani ya nchi kuwa ni zaidi ya milioni 600 lakini familia hiyo imekabidhiwa shilingi milioni 120 tu kitu ambacho wamekipinga vikali.

Kwa mujibu wa madai hayo, fedha za rambirambi zilizochangwa bila kupitia mikononi mwa familia hiyo ni zaidi ya milioni 600 huku milioni 345 zikichangwa kutoka nchini Ujerumani.

“Sisi kama wanafamilia tunajiweka mbali na ujumbe huo wa kizushi na wenye lengo la kutuchonganisha na Mwenyekiti wetu wa chama taifa, Freeman Mbowe,” amesema mbunge wa viti maalum wa chadema, Ruth Owenya.

Vilevile, ingawa hakutaka kutoa ufafanuzi, rambirambi zilizozua manung’uniko ni zile ambazo zilikuwa zimechangwa kwaajili ya wanafunzi na waalimu wa Lucky Vincent ya Jijini Arusha ambazo ni zaidi ya milioni 300.

Hata hivyo, Ndesamburo alifariki dunia Mei 31 mwaka huu alipofikishwa kutibiwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC iliyopo Moshi mini.

Joan Laporta: Nipo Tayari Kugombea Urais FC Barcelona
Paolo Maldini Kuwakabili Nadal, Federer, Djokovic