Familia ya marehemu Akwilina Akwiline imeridhia kuuchukua mwili wa marehemu mara baada ya madaktari wa Muhimbili kutoa ripoti kamili juu ya sababu zilizopelekea kifo cha aliyekuwa mwanafunzi wa NIT.

Taarifa hiyo imekuja baada ya ndugu wa marehemu kugoma kuuchukua mwili huo mpaka pale majibu ya daktari juu ya ripoti ya uchunguzi itakapokamilika na kuwekwa bayana kwa wanafamilia.

Hata hivyo familia imeridhia kuuchukua mwili wa marehemu na kuupumzisha katika nyumba yake ya milele.

Mmoja ya wanafamilia amesema ripoti ya madaktari imeeleza kuwa Akwilina alipata jeraha kichwani upande wa kulia na jeraha hilo kutokezea upande wa kushoto.

Ameongezea kuwa ”Tuliweza kumuona dokta na akatupa ukweli jinsi ulivyo, baada ya kupata ripoti kamili kama ndugu tuliridhika” Amesema mmoja wa familia.

Pia ameeleza kuwa kwa sasa wanampango wa kuelekea Moshi, kwani ndugu yao yupo Mochawri Muhimbili, baada ya mipango yote kukamilika marehemu AKwilina Akwiline atapumzishwa katika nyumba ya milele.

Mwili wa marehemu Akwilina utazikwa nyumbani kwao Kilimanjaro, wilaya ya Rombo, Marangu.

Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Februari 20, 2018
Chirwa awazodoa wanao mzushia