Familia ya rais wa awamu ya tatu, Hayati Benjamin Mkapa, leo Julai 26, 2020 imeweka bayana ugonjwa uliopelekea kifo chake usiku wa kuamkia Ijumaa Julai 24, 2020.

Msemaji wa familia hiyo wakati akitoa shukurani kwa waliofika kwenye ibaada ya kumwaga rais Mkapa, amesema baada ya kufanyiwa vipimo madaktari walibaini ana Malaria na alipokuwa anaendelea kupata matibabu alipata mshtuko wa moyo ambao ulipelekea umauti.

“Alikuwa hajisikii vizuri, akaenda hospitali akaonekana kwamba baada ya kuchukuliwa vipimo alikuwa na ugonjwa wa Malaria, akaanza matibabu na akalazwa siku ile ya jumatano”

Amesema wakati akiendelea kupata matibabu alikuwa anaendelea vizuri na anazungumza na wanafamilia huku akiangalia taarifa ya habari, ndipo alipopata mshtuko wa moyo na kufariki.

” Baada ya kusikiliza taarifa ya habari, aliinuka akitaka kutoka, alivyoinuka kukaa akainamisha kichwa na hiyo mpaka walivyokuja kumpima akawa amethibitika kwamba amefariki, sababu yake ya kifo alipata mshtuko wa moyo au kama wanavyoita kwa kitaalamu “cardiac arrest”. Amesema msemaji wa familia.

Aidha amebainisha kuwa familia imeamua kueleza chanzo hicho kwasababu kuna watu wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii kutaja sababu za kifo cha hayati Mkapa ambazo siyo sahihi na kuomba ukweli wa kifo chake alioutaja uheshimiwe, ampumzike kwa amani.

Somalia: Bunge lapitisha kumwondoa madarakani Waziri Mkuu
Video: Mwili wa Mkapa kutoka Lugalo - Uwanjani