Aliyewahi kuwa mshindi wa shindano la ulimbwende nchini (Miss Tanzania 2004), Faraja Kotta ameeleza jinsi alivyoguswa na mashambulizi ya mtandaoni dhidi ya Miss Tanzania mpya (2016), Diana Edward.

Miss Diana ameshambuliwa kuhusu umri wake kupitia mitandao ya kijamii, hali iliyosababisha waandaaji wa shindano hilo kutoa ufafanuzi ulionesha kuwa hata jina lililokuwa likitajwa kwenye mitandao hiyo pamoja na umri vilikuwa vya upotoshaji.

Faraja Kotta ambaye ni mke wa aliyewahi kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu ameandika ujumbe akikumbuka jinsi alivyoshambuliwa na baadhi ya vyombo vya habari siku moja baada ya kutajwa kuwa mshindi wa taji hilo.

Miss Tanzania 2016, Diana Edward

Miss Tanzania 2016, Diana Edward

Amelaani kitendo kinachofanywa dhidi ya Mrimbwende huyo mpya na kutoa wito kwa jamii kujikita katika kujenga zaidi ya kubomoa.

Huu ndio ujumbe aliouandika:

Niliposhinda Miss Tanzania, kuna mtangazaji fulani (tena wa kiume) wa kipindi cha redio cha asubuhi alitumia kama saa nzima hewani kusema ambavyo sikustahili kushinda. Asubuhi ya Jumatatu kama leo baada ya weekend ya shindano.

Nilipigiwa simu kuamshwa. Nakumbuka niliamka nikawasha redio na nikasikiliza kipindi chote, peke yangu, chumbani.

Nilitetemeka, nilishindwa kuoga, kula, nilijifungia ndani siku nzima nikilia. Niliwaza sana ambavyo pengine ni kweli sikustahili. Nilijuta kushiriki Miss Tanzania.

I was young and naive. I had just turned 19, coming straight from the safety nets of Catholic nuns boarding schools. Sikujua kuna watu wanaweza kuwa na roho mbaya hata kwa watu wasiowajua.

It took my parents (RIP) na kila busara waliyonayo kunifanya nijisikie vizuri. I had to dig deep inside me to regain my purpose. I was exposed to a cruel world and yes, I quickly learnt, it is what it is.

Leo hii hakuna binadamu mwenye hiyo nguvu niliyompa yule mtangazaji. I learnt the hard way but I am grateful for the lesson. Thank God I learnt early. Kuna sehemu ya nguvu niliyo nayo leo iliyotokana na kujeruhiwa na binadamu na kupona. Lakini si kila mtu atapata bahati ya kupona, unaweza kumjeruhi mtu na akapotea moja kwa moja. Usijitafutie laana za reja reja.

To the newly crowned Miss Tanzania, Do you honey!

To the rest of us, tujenge zaidi ya kubomoa. Love doesn’t cost a thing!

God bless,

Faraja

Manara: Sisi Hatuna Presha Na Hata MO Hana Presha
Jose Mourinho Hana Pakutokea, Kamati Yamsubiri Kwa Hamu