Rais anayemaliza muda wake wa Somalia, Mohamed Abdullahi Farmajo amekabidhi madaraka kwa Rais mpya wa nchi hiyo Hassan Sheikh Mohamud hii leo Mei 23, 2022.

“Namshukuru mwenyezi MUNGU leo ninakabidhi ofisi ya rais kwa rais mteule wa Shirikisho,” amesema Farmajo rais anayemaliza muda wake nchini Somalia.

Mara baada ya Rais huyo kukabidhiwa ofisi amesema analazimika kuongoza nchi hiyo inayokabiliwa na changamoto kadhaa kwa kupambana na ukosefu wa usalama unaosababishwa na kundi la Kiislamu la Al Shabaab.

“Kama rais alivyosema ninaomba watu wote wa Somalia popote walipo waniunge mkono na pia nawaomba kwa imani yenu kamili tushirikiane ili kufanikisha utatizi wa changamoto zinazotukabili,” amesisitiza Rais mteule.

Mohamud atalazimika kuongoza nchi hiyo inayokabiliwa na changamoto kadhaa kwa kupambana na ukosefu wa usalama unaosababishwa na kundi la Kiislamu la Al Shabaab.

Vilevile ana mtihani wa kukabiliana hali ya ukame wa kihistoria ambao umekuwa ukisababisha baa la njaa, vifo, kuwabili waasi na waislam wenye itikadi kali.

Katika uchaguzi wa nchi hiyo uliofanyika Mei 15 Mohamud alimshinda Farmaajo kwa kupata kura 214 dhidi ya kura 110 za mwisho katika duru ya tatu.

Wakandarasi wababaishaji kupigwa buti na Serikali
CHADEMA kutoshiriki mchakato wa kutoa maoni