Siku ya mtoto wa Afrika imekuwa ikisherehekewa toka mwaka 1991 tarehe 16 ya mwezi wa 6. Mwaka huu 2016 siku hii inasherekewa ikiwa na kauli mbiu ya “Migogoro ndani ya Afrika; Tulinde haki zote za watoto”

Kauli mbiu hii inakuja wakati ambapo baadhi ya nchi za Afika zimekuwa katika migogoro ya muda mrefu bila suluhisho la kudumu. Hivyo katika kuadhimisha siku hii, Afrika inakumbushwa kwamba inawezakana kumaliza migogoro na hivyo kuwafanya watoto wa Afrika kuishi maisha salama kama watoto waishio katika mabara mengine.

Fastjet ikiwa ni kati ya mashirika ambayo yamekuwa yakifanya kazi na jamii katika kuhakikisha watoto wanakua katika mazingira bora huku wakipata huduma zote muhimu pamoja na za kiafya, wanasherehekea siku hii kwa kutembelea kituo cha watoto yatima kilichopo Moshi, Mabogini na kusikiliza mahitaji yao mbalimbali na kutoa misaada.

Afisa Uhusiano na Masoko wa Fastjet Lucy Mbogoro amesema kuwa Fastjet imekuwa Karibu sana na jamii hasa watoto, ambapo katika miaka yake mitatu toka shirika lianzishwe hapa Tanzania, shirika limeweza kutoa misaada mbalimbali kwa vituo kadhaa vya watoto yatima na pia limeweza kusafirisha madaktari zaidi ya 20 kuelekea vituo mbali mbali kwaajili ya kutoa huduma za kiafya au upasuaji kwa watoto wenye mahitaji ambao walishindwa kufika kwenye hospitali zetu kubwa zilizopo mijini.

FastJet

Aidha Lucy aliendelea kwa kusema kuwa Fastjet inakaribisha maombi mbalimbali kutoka kwa madaktari ambao wanatarajia kwenda kutoa huduma za kiafya kwa watoto katika vituo ambayo fstjet inafika, ili kuwapa huduma bora, pia shirika litahakikisha linaendelea kushirikiana na madaktari ili kulinda afya za watoto na maisha yao kwa ujumla.

 

TCRA kumaliza kazi yao kesho.
Prof. Ndalichako aingia ndani ya bodi ya mikopo.