Mwanasheria na wakili wa kujitegemea, Fatma Karume amefunguka kuhusu uamuzi uliotolewa na Jaji Mkuu wa mahakama kuu nchini, Dr. Eliezer Feleshi juu ya kumsimamisha uwakili kwa kipindi cha muda usiojulikana kufuatia kesi aliyokuwa anaisimamia ya mteja wake Ado Shahibu aliyefungua shitaka dhidi ya Rais John Pombe Magufuli.

Fatma amelalamika kuwa hatua hizo zimechukuliwa bila kufuata taratibu kwani ilitakiwa kabla ya kufanyika kwa uamuzi huo alitakiwa aitwe na aweze kutoa sababu zake kwa nini asichukuliwe hatua.

”Nimesikia kwamba nimevuliwa uwakili mpaka pale anavyosema yeye jaji Feleshi, nimefutiwa kwa muda mpaka pale kesi yangu ikisikilizwa na advocate comittee, kuna tatizo kubwa na hiyo ‘order’ yake, huwezi ukatoa msitisho wa muda wakati kesi haijapelekwa mahakamani, hakuna mtu aliyenipeleka kwenye kamati, hajafuata taratibu za kisheria, Pia Kuna utaratibu mwingine lazima ufuatwe huwezi ukatoa order ya kumsitisha mtu bila ya kusikia upande wake, angeweza kuniita na anisikilize na au aniulize kwa nini aitoe order hii” amesema Fatma karume.

Aidha, Fatma amesema kwamba haoni haja ya kupingana na uamuzi huo, ila hajastaajabu maamuzi yaliyofanywa na mahakama kwani yeye ataendelea kuwa wakili, ‘mimi bado ni Advocate’ sauti ya Fatma ilisikika hivyo.

Aidha anasema kuwa lengo lake kubwa lilikuwa ni kuleta mabadiliko kwa kutumia sheria, na hiyo ndio sababu amefanya uthubutu wa kumpeleka Rais Mahakamani kwa lengo la kumtaka afuate katiba.

”Nimethubutu kumchukua rais mahakamani nimethubutu kuchukua kesi ya Ado kumpeleka rais mahakamani ili kuhakikisha anafata katiba yetu feleshi ananishughulikia”. Ameongezea Karume.

Mapema jana Fatma Karume alisimamishwa uwakili na ajaji Mkuu kutoka Mahakama kuu ya nchi, Feleshi ambapo upande wa serikali umelalamikia matamshi yaliyotolewa na wakili huyo katika kesi hiyo iliyofunguliwa dhidi ya Rais John Pombe Magufuli na mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Mbaroni kwa kukutwa na nyama ya wanyama pori
Aliyetumiwa pesa kimakosa ashtakiwa kwa wizi