Rais wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika, TLS na Wakili wa Kujitegemea, Fatma Karume amesema kuwa yuko tayari kuitwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa ajili ya kutoa elimu ya masuala ya Katiba na sheria za nchi.

Ameyasema hayo Jijini Dar es salaam mara baada ya kuonekana kwake kwenye kikao cha vyama 6 vya siasa vya upinzani nchini mkutano ambao ulifanyika Zanzibar na kutoa maazimio mbalimbali.

“Mimi nilialikwa na vyama vya upinzani kuwapa mafunzo juu ya Katiba yetu, ili waelewe wanachokijadili kuhusu katiba yetu, lakini pia nikialikwa na CCM kuwaeleza kuhusu Katiba nitawaeleza kila mwanasiasa akitaka kujua katiba yetu tutaishi maisha bora zaidi.”amesema Fatma Karume

Aidha, ameongeza kuwa yeye hafungamani na chama chochote, hivyo vyama vya CCM, CUF, CHADEMA, ACT- Wazalendo yuko tayari kutoa msaada wa kisheria au kikatiba kuhusu haki za vyama.

Hata hivyo, ameongeza kuwa yuko tayari kutoa msaada wowote wa mafunzo ya kisheria ndani ya chama tawala CCM pindi tu watakapo mhitaji kwa ajili ya huduma hiyo, huku akiksisitiza kuwa mafunzo hayawezi kubadili msimamo wake.

LIVE: Rais Magufuli akiwatunukia vyeo waliofanya vizuri zaidi mafunzo ya uofisa na ukaguzi
LIVE: Rais Magufuli akiwatunukia vyeo waliofanya vizuri zaidi mafunzo ya uofisa na ukaguzi

Comments

comments