Gwiji wa soka nchini Colombia Faustino Hernán Asprilla Hinestroza amemtuhumu mshambuliaji Cristiano Ronaldo kwa kusema anachangia kuua kipaji cha James Rodriguez.

Asprilla ambaye aliwahi kutamba na klabu Newcastle United ya nchini England, amesema Ronaldo amekua hampi ushirikiano wa kutosha James wanapocheza kwa pamoja katika kikosi cha Real Madrid.

Amesema Ronaldo amekua na ubinafsi wa kutaka kufunga mwenyewe na wakati mwingine hushindwa kutoa hata pasi ya mwisho kwa James, jambo ambalo linaendelea kumshusha nahodha huyo wa kikosi cha Colombia.

Gwiji huyo wa soka la Colombia amezungumzia suala hilo kufuatia James kuonyesha kiwango duni wakati wa michezo ya kuwania nafasi ya kucheza fainali za kombe la dunia dhidi ya Chile, jambo ambalo lilisababisha kuachwa nje ya kikosi kilichopambana na Argentina waliochomoza na ushindi wa mabao matatu kwa sifuri.

“Kucheza sambamba na Cristiano Ronaldo kunahitaji moyo wa uvumilivu, ninamshauri James kuwa na subra kwa sababu kuna makusudi ya dhahir anafanyiwa na mchezaji huyo wanapocheza kwa pamoja wanapokua Real Madrid.” Asprilla aliiambia ESPN.

“Ronaldo ni mbinafsi naamini hata wadau wengine wa soka wanalitambua hilo, sasa ni vigumu kuona mchezaji kama James anang’aa katika soka la sasa, kwa hiyo mimi naendelea kumsihi awe na subra.

Video: Ommy Dimpoz amkejeli Nay wa Mitego kwa majanga yaliyompata
Video: Waziri awataka Machinga kutii sheria bila shuruti