Mgombea wa Urais kupitia muungano wa vyama vya upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Martin Fayulu amewataka wafuasi wake kuandaa maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais baada ya Mahakama ya Katiba kukataa shauri lake la kukataa matokeo hayo.

Mgombea wa upinzani Felix Tshisekedi tayari Jumamosi alitangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa Disemba 30, 2018.

Aidha, vyanzo vya habari nchini DRC vimesema kuwa Fayulu anaendelea kudai kuwa Tshisekedi alifanya makubaliano ya kuunda serikali ya pamoja na rais anaye ondoka madarakani, Joseph Kabila lakini timu ya uchaguzi ya Tshisekedi inakanusha hilo.

Hata hivyo, wafuasi wa Tshisekedi walijitokeza katika mitaa ya jiji la Kinshasa baada ya uamuzi wa Mahakama mapema majira ya asubuhi Jumapili kusheherekea ushindi wao.

 

Video: CAG kikaangoni, Zitto ageuka Mtikila
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Januari 21, 2019

Comments

comments