Mkurugenzi wa Mkuu wa  (FBI),nchini Marekani  James Comey ameliambia bunge la Marekani kuwa baada ya kupitia barua pepe zilizogundulika kutoka kwa Hillary Clinton, wakati alipokuwa Waziri wa mambo ya nje wamegundua kuwa hana hatia yoyote na hawatamfungulia mashtaka.

Kampeni za Clinton ziliingia kwenye kashifa wiki iliyopita mara baada ya Mkurugenzi huyo wa FBI kusema kuwa watazipitia barua pepe zake zilizopatikana katika kompyuta ya msaidizi wa zamani wa mume wake.

Wakati   Clinton akifurahia hatua hiyo kwa upande wake Donald Trump amesema Hillary Clinton analindwa na mfumo wa wizi wa kura, na  anatakiwa kuchunguzwa kwa muda mrefu.

Cristiano Ronaldo, Florentino Perez Wakubaliana
Video: Makonda kujenga vituo ishirini vya polisi jijini Dar