Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC kupitia kipindi chake maalumu cha uchunguzi, limeuona ushahidi kwamba rais wa FIFA Sepp Blatter aliyesimamsishwa kwa muda anachunguzwa na shirika la ujajusi la Marekani FBI kuhusiana na hongo ya dola milioni 100.

Kampuni ya masoko ya michezo inaaminika kulipa mamilioni ya dola za Kimarekani kwa maafisa waandamizi wa FIFA katika miaka ya mwishoni mwa 1990 ili kupewa haki ya kutangaza michuano ya kombe la dunia.

Aliyekuwa ameshika nafasi hiyo kabla ya Blatter, Joao Havelange, alikuwa ni mmoja wa wanaotuhumiwa kupokea malipo hayo.

Blatter, amekana kuwa na taarifa yoyote ya sakata hilo, lakini kipindi cha Panorama kimeona barua iliyosainiwa na Joao Havelange ikisema  Blatter anazo taarifa kamili.

Mayweather Aonyesha Anavyoponda Raha
Ulimwengu, Samatta Watua Japan