Mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na nahodha na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi katika dakika ya 90, uliisaidia FC Barcelona kupata ahuweni ya matokeo katika mchezo wa ligi ya nchini Hispania dhidi ya Villarreal usiku wa kuamkia hii leo.

Villarreal ambao walikua nyumbani katika uwanja wa El Madriga, walitangulia kupata bao katika dakika ya 50 kupitia kwa Nicola Sansone.

Kwa matokeo hayo FC Barcelona wameendelea kuwa na wakati mgumu wa kuwafukuza vinara wa msimamo wa ligi ya nchini Hispania Real Madrid, ambao walichomoza na ushindi mnene siku ya jumamosi dhidi ya Granada wa mabao matano kwa sifuri.

FC Barcelona wameshuka hadi katika nafasi ya tatu wakimiliki point 35, nafasi ya pili inashikiliwa na Sevilla wenye point 36 na Real Madrid wana point 40.

Real Madrid bado wana mchezo mmoja mkononi na kama watafanikiwa kushinda wataendelea kujikita kileleni.

Matokeo ya michezo mingine ya ligi ya nchini Hispania iliyochezwa jana.

Athletic Bilbao 0 – 0 Alaves

Real Betis 2 – 0 Leganes

Celta Vigo 3 – 1 Malaga

Didier Drogba Abisha Hodi Stade Vélodrome
Rais Shein awapa ‘neno’ wanaofikiri ataondolewa madarakani na UN