Uongozi wa FC Barcelona umesitisha zoezi la kuachana na meneja wa kikosi cha klabu hiyo Ronald Koeman, kwa kuhofia kumlipa fedha nyingi kama fidia za kuvunja mkataba wake.

Koeman amekua katika wakati mgumu klabuni hapo kufuatia kikosi chake kuwa na matokeo mabaya, jambo ambalo liliibua minong’ono huenda akatimuliwa kazi wakati wowote.

FC Barcelona haiwezi kumfukuza Koeman mwenye umri wa miaka 58 bila kumlipa karibu pauni milioni 10 kama fidia ya kuvunja mkataba wake.

Hata hivyo kama mambo yataendelea kuwa mabaya kwa meneja huyo kutoka nchini Uholanzi, huenda akapewa muda wa mwezi mmoja, na kama atashindwa kufikia lengo, ndipo ataonyeshwa mlango wa kutokea.

Aliyewahi kuwa meneja wa klabu hiyo Roberto Martinez anatajwa na Bodi ya Barca kuchukua nafasi ya Koeman, endapo atashindwa mtihani unaomkabili kwa sasa.

Barcelona itacheza mechi ya LaLiga ugenini leo dhidi ya Cadiz, halafu itarejea nyumbani Nou Camp Septemba 26, mwaka huu kuwakaribisha Levante.

Barca itakuwa mgeni wa Benfica ifikapo Septemba 29, mwaka huu katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kabla ya kuwavaa mabingwa wa Hispania Athletico Madrid katika La Liga hapo Oktoba 2, mwaka huu.

Waziri Nchemba: Msiwaingilie wakaguzi wa ndani
Eto'o kuwania Urais Cameroon