Rais wa mabingwa wa soka nchini Hispania FC Barcelona Josep Maria Bartomeu, ameanza mikakati ya kutaka kuzungumza na wakala wa mshambuliaji kutoka Ufaransa Antoine Griezmann, ili kukamilisha ndoto za kumuhamishia Camp Nou msimu ujao.

Bartomeu amekiambia kituo cha Radio cha RAC1: “Tunakamilisha taratibu za mwishoni mwa msimu huu, tutaangalia namna ya kuanza mipango ya usajili wa Griezmann.

“Nimeshafanya mawasilino ya awali na wakala wake, na wakati wowote tutakutana ili tuzungumzie jambo hili, maana ninataka limalizwe mapema.

“Pia niliwahi kuzungumza kwa kifupi na rais wa Atletico Madrid Enrique Cerezo kuhusu jambo hili, lakini mazungumzo yetu hayakwenda mbali sana.”

Griezmann anapewa nafasi kubwa ya kuondoa Wanda Metropolitano mwishoni mwa msimu huu, kufuatia kiwango chake kuwaridhishwa viongozi wa FC Barcelona.

Hata hivyo endapo FC Barcelona watakubaliwa kuanza mazingumzo ya uhamisho wa mshambuliaji huyo, watalazmika kulipa ada ya Pauni milioni 87 sawa na Euro milioni 100, na hii ni kutokana na vifungu vilivyopo kwenye mkataba wa Griezmann.

Mwezi Machi Griezmann waliwahi kusema, anahitaji kufanikisha ndoto za kuondoka Atletico Madrid kabla ya kwenda nchini Urusi kushirikki fainali za kombe la dunia, akiwa na timu yake ya taifa ya Ufaransa.

Fahamu vigezo vilivyotolewa na HESLB kwa waombaji wa mkopo elimu ya juu
Massimiliano Allegri, Luis Enrique wachuana vikali