Beki wa kulia kutoka nchini Ivory Coast na klabu ya PSG ya Ufaransa Serge Aurier, anahusishwa na mipango ya kutaka kusajiliwa na FC Barcelona.

Jarida la France Football, limeeleza mlolongo wa beki huyo kuwa katika mipango hiyo, kwa kumuhusisha wakala kwake ambaye anadaiwa kuanza mazungumzo na viongozi wa FC Barcelona.

Stephan Courbis ambaye ni wakala wa Aurier, anadaiwa alikuwa mjini Barcelona kwa ajili ya kuzungumza na viongozi wa klabu bingwa nchini Hispania na amewaeleza uwezekano wa suala hilo kufanikiwa, lakini akaweka wazi changamoto za kuvunja mkataba wa mchezaji na PSG wake ambao utafikia kikomo mwaka 2019.

Aurier amekua mmoja wa wachezaji bora wanaocheza nafasi ya ulinzi wa kulia duniani, jambo ambalo FC Barcelona wanaamini litasaidia kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Dani Alves aliyetimkia kwa mabingwa wa soka nchini Italia Juventus FC.

Ligi Kuu Tanzania Bara Raundi Ya 15
Taifa Stars Itakayocheza Na Zimbabwe Yatangazwa