Mshambuliaji wa Brazil na klabu ya Barcelona Neymar ambaye ametoka kuiongoza timu yake ya taifa kutwaa medali ya dhahabu kwa mara ya kwanza kwenye Michuano ya Olimpiki, ameongezewa muda wa mapumziko na klabu yake na hivyo kuukosa mchezo wa wikiendi dhidi ya Athletic Bilbao
Mapumziko hayo yatamalizika baada ya mechi za kimataifa ambapo itakuwa ni wiki ya pili ya mwezi Septemba.
Neymar atakuwepo kwenye kikosi cha Brazil kitakachoivaa Ecuador na Colombia mwanzoni mwa mwezi Septemba.
Hiki kinakuwa kikosi cha kwanza kabisa kwa kocha Tite ambaye aliteuliwa kurithi mikoba ya Dunga aliyetimuliwa baada ya matokeo mabovu.
Mbali na Neymar, ambaye alitangaza kujivua unahodha baada ya kumalizika kwa Michuano ya Olimpiki, pia wamo Gabriel Barbosa na Gabriel Jesus ambao waling’ara Kikosi cha Olimpiki cha Brazil na Tite ameteua wachezaji sabab kutoka Kikosi hicho cha Mabingwa wa Olimpiki.
Wengine toka Kikosi hicho cha Olimpiki ambao wameitwa Brazil ni Kipa wa Atletico Paranaense, Weverton, Kiungo wa Beijing Guoan, Renato Augusto ambao pamoja na Neymar ndio walikuwa Wachezaji Watatu waliozidi Miaka 23 kuwemo Olimpiki.
Wawili wengine kutoka Olimpiki ni Marquinho na Rodrigo Caio.
Gabriel Jesus, ambaye amejiunga na Chelsea hivi karibuni, atakuwa akiichezea Brazil kwa mara ya kwanza.

 

Mamadou Sakho Arejea Mazoezini Liverpool
TFF Yaiandalia Serengeti Boys Kambi Tulivu