Mshambuliaji wa klabu bingwa nchini Hispania FC Barcelona Paco Alcacer amejiunga na klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani kwa mkopo hadi mwishoni mwa msimu huu, huku mkataba wake ukumpa nafasi ya kusajiliwa moja kwa moja endapo ataonyesha kiwango kitakachoridhisha.

FC Barcelona na Borussia Dortmund wamefikia makubaliano hayo, huku ada ya kusajiliwa jumla kwa mshambuliaji huyo ikitajwa kufikia Euro milioni 28.

“Borussia Dortmund  imelipa kiasi cha Euro milioni 2 kwa ajili ya usajili wa mkopo wa muda mrefu wa Paco Alcacer,” Imeeleza taarifa iliyotolewa na mabingwa hao wa Hispania.

“Ni matarajio yetu kuona mshambuliaji huyu anaendelea kucheza soka kwa kiwango cha juu akiwa na klabu ya Dortmund, tunaamini atafanikisha mpango wake wa kuwa kwenye kiksoi cha kwanza hadi mwishoni mwa msimu huu.”

“Tumeafiki kumuuza jumla endapo Dortmund watapendezwa na kiwango chake, lakini kama itakua tofauti watamrudisha kama mkataba tuliosaini unavyoeleza”.

Alcacer, ambaye atafikisha umri wa miaka 25 kesho alhamisi, alijiunga na FC Barcelona akitokea Valencia CF mwaka 2016, lakini ameshindwa kufikia kiwango kinachomuwezesha kuingia kwenye kikosi cha kwanza cha klabu hiyo ya Camp Nou, kwa kushindana na washambuliaji Luis Suarez na Lionel Messi.

Mshambuliaji huyo anaondoka FC Barcelona huku akiwa ameweka historia ya kufunga mabao 15 katika michezo 50 aliyocheza kwa misimu miwili, na ameshinda taji moja la ligi (La Liga), kombe la Mfalme (Copa del Rey) mara mbili na kombe la Hispania (Spanish Super Cup) mara moja.

Neno la Simbachawene baada kumrithi Ghasia
Askari wawili wafukuzwa kazi