Hatimae FC Barcelona wamekubali kuvunja mkataba na beki Martin Montoya, baada ya kushindwa kumshawishi kuendelea kubaki Camp Nou kwa ajili ya shughuli za kusaka mafanikio ya msimu wa 2016/17.

Montoya amelazmika kukubali kuvunjwa kwa mkataba wake, baada ya kuchoshwa na hatua ya kushindwa kupata nafasi katika kikosi cha kwanza, jambo ambalo limekwenda kinyume na matarajio yake ya muda mrefu.

Beki huyo ambaye ni zao la FC Barcelona kutoka kwenye kituo chao cha kulea na kukuza vijana cha La Masia, amekua na bahati mbaya kwa mameneja wote waliopita klabuni hapo tangu mwaka 2011, kwani mpaka mkataba wake unavunjwa alikua amecheza michezo 66 pekee.

Hata hivyo FC Barcelona walijitahidi kumpeleka kwa mkopo katika klabu za Inter Milan na Real Betis, lakini bado imeonekana kupatikana kwa nafasi kwa beki huyo imekua tatizo kubwa.

Maamuzi ya kuvunjwa kwa mkataba wa Montoya mwenye umri wa miaka 25, yameinufaisha klabu ya Valencia CF ambayo imetangaza kumsajili na kumuhakikishia kucheza karibu kila mwishoni mwa juma.

Valencia CF wametangaza kumsajini Montoya na wanaamini atawasaidia katika harakati zao za mapambano ya msimu mpya wa ligi ya nchini Hispania, ambayo yaatanza rasmi mwishoni mwa mwezi huu.

Southampton Wasajili Mwingine Kutoka Ufaransa
SSC Napoli Wapata Mbadala Wa Gonzalo Higuain