Kikosi cha klabu ya Valencia kinachonolewa na beki na nahodha wa zamani wa Man Utd, Gary Neville usiku wa kuamkia hii leo kilipata wakati mgumu mbele ya FC Barcelona baada ya kukubali mabao saba kwa sifuri katika mchezo wa kombe la Mfalme (Copa del Rey).

Mchezo huo wa mkondo wa kwanza, ulishuhudia mabao ya FC Barcelona yakipachikwa wavuni na mshambuliaji kutoka nchini Uruguay, Luis Suarez aliyefunga mabao manne, huku nyota wa Argentina Lionel Messi akifunga mabao matatu.

Barcelona's Luis Suarez shoots to score a goal against Valencia's Aderlan SantosLuis Suarez

Hata hivyo mshambuliaji kutoka nchini Brazil, Neymar hakufanikiwa kufunga katika mchezo huo, na badala yake alikosa mkwaju wa penati.

Lionel Messi akiwa na Neymar

Valencia walionekana kuishiwa nguvu ya ushindani, baada ya beki wao kutoka nchini Ujerumani, Shkodran Mustafi kuonyeshwa kadi nyekundu kufuatia mchezo mchafu aliouonyesha dhidi ya Lionel Messi.

Kufungwa kwa kikosi cha Valencia, kunaendeleza hatua ya Gary Neville kutokupata ushindi katika michezo yote minane iliyoshuhudia akikaa katika benchi la ufundi tangu alipopewa majukumu mwezi Disemba mwaka 2015.

Akizungumza mara baada ya mchezo huo dhidi ya Barcelona, Neville alisema siku hiyo ni moja ya siku zenye machungu zaidi katika maisha yake katika ulimwengu wa soka.

Chelsea Wabanwa Mbavu Na Watford
Picha: shabiki Yanga Apoteza Fahamu Baada Prisons Kupachika Bao La Pili