Kiungo kutoka nchini Ureno Renato Sanches, amejiunga na mabingwa wa soka nchini Ujerumani FC Bayern Munich akitokea Benfica.

Kiungo huyo alioyekua anahusishwa na mipango ya kujiunga na klabu ya Man Utd ya nchini England, amekamilisha mpango wa kuelekea Allianz Arena muda mcheche uliopita kwa ada ya uhamisho inayokadiriwa kufikia Pauni million 28.

Sanchez amejiunga na mabingwa hao na kukubali kusaini mkataba wa miaka mitano ambao utamuweka mjini Munich hadi mwaka 2021.

Mtendaji mkuu wa FC Bayern Munich, Karl-Heinz Rummenigge amethibitisha taarifa hizo kupitia mndao wa klabu hiyo, kwa kusema imekua furaha na faraja kwa kila moja klabuni hapo kutokana na kukamilisha mpango wa kumnasa kinda huyo.

Amesema wanaamini Sanchez ataweza kuisaidia klabu hiyo kuendelea kufikia malengo yaliyokusudiwa kuanzia msimu ujao wa ligi ambapo wamedhamiria kutwaa ubingwa wa barani Ulaya, baada ya kujaribu kwa misimu mitatu mfululizo na kujikuta wakiishia katika hatua ya nusu fainali.

Sanchez, atajiunga rasmi na FC Bayern Munich mara baada ya msimu wa 2015-16 kuhitimishwa majuma mawili yajayo.

Lionel Messi Awaombea Njaa Real Madrid
11 Wa Kwanza Dhidi Ya Yanga Hawa Hapa