Klabu ya FC Platinum na Bulawayo Chiefs zote za Zimbabwe ziko katika mvutano kuhusu usajili wa Perfect Chikwende aliyesajiliwa na klabu ya Simba ya Tanzania na kupelekea kuchelewesha kutolewa kwa hati ya uhamisho wa kimataifa (ITC) ya mshambuliaji huyo.

Chikwende alisaini mkataba wa miaka miwili na Simba lakini bado hajapata ITC yake baada ya klabu yake ya zamani, Bulawayo Chiefs kukiandikia Chama cha Soka cha Zimbabwe kusitisha mchakato wa kutoa ITC kwa madai ya kwamba FC Platinum inapaswa kuwafidia kwa kuwa walimtoa kwa mkopo Chikwende kwenda FC Platinum.

Chikwende alipelekwa kwa mkopo FC Platinum kwa msimu wa 2019/20 lakini kwa sababu ya Ligi kusimama kutokana na  Covid-19, Chama cha Soka Zimbabwe kilitoa muongozo kikifafanua kwamba mikataba ambayo ilikuwa ikimalizika mnamo 2020 inapaswa kuendelea hadi 2021.

Bulawayo Chiefs wanadai wana haki ya kulipwa sehemu ya dau la uhamisho lililolipwa FC Platinum na klabu ya Simba kwa FC Platinum.

Peter Muduhwa atambulishwa Simba SC
Baraza la Seneti lapokea hati ya mashtaka dhidi ya Trump