Msemaji wa FC Platinum, Chido Chizondo amethibitisha taarifa za kuondoka kwa mshambuliaji Perfect Chikwende, ambaye anahusishwa na taarifa za kuwaniwa na mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba SC.

Chizondo akiwa  kwenye mahojiano na chombo kimoja cha habari mjini Harare, Zimbabwe amesema mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 amesafiri kuelekea Dar es salaam, Tanzania.

Hata hivyo Chizondo hajaweka wazi mshambuliaji huyo ameelekea Dar es salaam kwa mpangowa kujiunga na klabu gani, licha ya mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba SC kupewa kipaumbele, huku Azam FC wakihusishwa kwenye dili hilo.

“Hatuwezi kuthibitisha kuwa ni klabu gani ameenda kujiunga nayo lakini tunaweza kusema kuwa ameondoka na kwenda Tanzania,”

“Simba wameweka mezani ofa lakini pia Azam FC nao wanaonekana kuvutiwa naye, tunasubiri kuona matokeo.” Amesema Chizondo.

Ripoti zinasema Simba wapo watayari kutoa  Dola 55 000 ambazo ni zaidi ya sh 127 milioni  kwa ajili ya kupata huduma  mshambuliaji huyo wa zamani wa  Bulawayo Chiefs , lakini  Azam FC nao wanatajwa kuwa kwenye nafasi nzuri ya kumnasa nyota huyo.

NECTA yatangaza matokeo ya kidato cha nne 2020
Raphael Daudi anaswa Ihefu FC