Saa 48 zikisalia kabla mchezo wa hatua ya mzunguuko wa pili ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, kati ya FC Platnum dhidi ya Simba SC, wenyeji wa mchezo huo wameanika mipango na mikakati ya kujitengeneza mazingira mazuri ya kutinga hatua ya makundi.

FC Platnum watakua wenyeji wa mchezo wa mkondo wa kwanza utakeochezwa keshokutwa Jumanato (Desemba 23), kwenye Uwanja wa National Sports kuanzia saa 10 jioni kwa saa za  Tanzania na saa 9 Alasiri kwa saa za Zimbabwe.

Msemaji wa FC Platnum, Chido Chizondo amesema wamejiandaa vizuri kwa kuhakikisha wanapata matokeo makubwa katika mchezo huo kwa kuwa wanatambua ubora wa Simba inapocheza kwenye uwanja wake wa nyumbani.

“Tumejiandaa kupata matokeo mazuri, namaanisha ushindi mkubwa ambao kwetu hauwezi kuwa kikwazo katika mchezo wa marudiano, tunajua kwamba Simba ni bora lakini tutakuwa bora kwa sababu tunaanzia kwetu.”

“Nadhani kikubwa ni kwamba tunaelewa Simba ni timu ya aina gani kutokana na kuweza kutumia vyanzo vyetu kufahamu baadhi ya mambo muhimu lakini tunaelewa kuna baadhi ya maofisa wao wameshaingia Zimbabwe ila hatuwezi kuhofia chochote.” Amesema Chizondo.

FC Platinum inayotumikiwa na mshambuliaji kutoka nchini Tanzania, Elias Maguri ilitinga hatua ya mzunguuko wa pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kuifunga Costa do Sol ya Msumbiji jumla ya mabao manne kwa moja, huku Simba SC wakiishinda Plateau United ya Nigeria kwa bao moja kwa sifuri.

Nandy, Dj Sinyorita, Rayvvan na Diamond Platnumz wangara tuzo za AEAUSA
Abiria wa Uingereza wapigwa marufuku kuingia mataifa ya Ulaya