Beki wa pembeni (Kulia) kutoka nchini Ureno Diogo Dalot, anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya juma hili ili kukamilisha usajili wa kujiunga na Man Utd, akitokea FC Porto.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na kituo cha televisheni cha Sky Sports zinaeleza kuwa, uongozi wa FC Porto umekubali kumuachia Dalot kwa ada ya Pauni milioni 17.4 sawa na Euro milioni 20.

Meneja wa Man Utd Jose Mourinho, amekua mstari wa mbele kuhakikisha usajili wa beki huyo mwenye umri wa miaka 19, unakamilika ili kufanikisha mpango wa kuwa na mtu wa kuaminika katika nafasi ya ulinzi wa kulia kwenye kikosi chake.

Wakati mpango wa Dalot ukiwa njiani kukamilika, Man Utd wakati wowote wanatarajiwa kumtangaza kiungo kutoka nchini Brazil Fred, ambaye jana alifanyiwa vipimo vya afya jijini Manchester.

Fred yu njiani kujiunga na Mashetani wekundu akitokea Shakhtar Donetsk ya nchini Ukraine, kwa ada ya Euro milioni 50.

Aswekwa rumande kwa kumdanganya kiongozi wa mbio za Mwenge
Video: Simulizi chungu ya Maria na Consolata kutoka Muhimbili, Wabunge hatarini kukamatwa