Uongozi wa klabu ya Yanga, umesema fedha zinazotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan zimeongeza ari kubwa kwa wachezaji kuipigania timu yao.

Mratibu wa Yanga, Hafidh Salehe ameyasema hayo wakati wa uchezeshaji wa droo ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam hatua ya robo fainali, iliyofanyika katika ofisi za Azam Media jijini Dar es salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Amesema, kipindi cha nyuma timu yao ilikuwa inaishia hatua ya awali ya michuano ya Kimataifa, lakini sasa vijana wamekuwa na hamasa kubwa ya kuipigania nembo ya timu yao na kuongeza kuwa, “tunashukuru kwa hamasa hii, wachezaji wanapambana kuipatia timu matokeo mazuri uwanjani, tunashukuru kwa kila kitu kinachochangia ushindi wetu.

Kikosi cha Timu ya Yanga.

“Historia imebadilika na wakati huu tunaenda kwenye mechi ya mwisho wa wiki tukiwa na shauku kubwa ya kuona timu yetu inashinda mbele ya wageni wetu US Monastir, mchezo utakaopigwa siku ya Jumapili katika Uwanja wa Taifa wa Benjamini Mkapa, jijini Dar es Salaam,” Alisema.

Klabu za soka za Yanga na Simba, zinaogelea Bahari ya fedha za Rais Samia, aliyeahidi kununua kwa Shilingi Milioni 5 kila goli linalopatikana, wakati timu hizo zinaposhiriki michezo katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho.

Uteuzi Makatibu Tawala, uhamisho wa vituo vya kazi
Ramaphosa, Samia wazungumzia Biashara, uwekezaji