Kiungo Mshambuliaji wa Young Africans Feisal Salum ‘Fei Toto’ amesema hatochoka kuisaidia timu yake kusaka alama tatu muhimu za kila mchezo wa Ligi Kuu msimu huu 2021/22.

Fei Toto tayari ameshaifungia Young Africans mabao mawili katika michezo mitatu aliyocheza msimu huu, huku akionesha uwezo mkubwa ambao unaendelea kuwa gumzo miongoni mwa Mashabiki na Wanachama wa klabu hiyo.

Kiungo huyo kutoka visiwani Zanzibar amesema kazi yake ni kucheza soka, na siku zote anapopewa nafasi kwenye kikosi cha timu yake hufikiria namna ya kutoa msaada kwa wengine, na kufunga kama nafasi itajitokeza.

“Kazi yangu mimi ni mpira na nikiwa uwanjani huwa ninafikiria kufunga ama kutengeneza nafasi ya kufunga kwa mwenzangu kwani kila tunapoingia uwanjani tunahitaji ushindi.

“Sipati tabu kwenye kufunga kwa kuwa kwenye kila mazingira huwa ninakuwa ninajua hapa ninapaswa nipige mpira kwa mtindo gani inakuwa rahisi kwa sababu ni vitu ambavyo ninavifanyia mazoezi mara kwa mara,” amesema Feisal Salum ‘Fei Toto’.

Mabao mawili aliofunga Feisal Salum ‘Fei Toto’ msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ilikua dhidi ya Kagera Sugar mjini Bukoba mkoani Kagera na KMC FC mjii Songea mkoani Ruvuma.

Simba SC vs Polisi Tanznaia
Simba SC yatolewa mbio za ubingwa 2021/22