Licha ya kuwa na kizazi ambacho kimepachikwa jina la kizazi cha dhahabu ‘golden generation’, lakini Ubelgiji wamekuwa hawafanyi vizuri katika michuano mikubwa.

Hawakufanya vizuri katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2014 na pengine lingepaswa kuwa somo kwa ajili ya michuano ya Euro mwaka huu.

Hata hivyo hali imekuwa tofauti badala yake wameanza tena vibaya baada ya kupokea kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Italy ‘Azzurri’.

Na kutokana na kipigo hicho mashabiki mbalimbali kupitia mtandao wa Twitter wamekuwa wakiwaangushia mzigio wa lawama baadhi ya wachezaji.

Baadhi ya wachezaji waliogeuka ‘case study’ ni Romelu Lukaku na Marouane Fellaini ambao wamepigwa ‘madongo ya kufa mtu’

 

Baadhi ya tweet zinazowaponda hizi hapa

 

 

Hizi Hapa Sababu Za Kufutwa Kwa Umitashumta Na Umisseta
Makala: Filamu ya Soka ya Brazil inaumiza macho