Nahodha na Mashambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania ‘TAIFA STARS’ Mbwana Ally Samatta huenda akaondoka Fenerbahce ya Uturuki, kufuatia kiwango chake kutoridhisha.

Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika kutoka nchini Uturuki, ambacho kimefichua ukweli wa mambo, kimeripoti kuwa Fenerbahce wameanza mipango ya kutaka kumpiga bei mshambuliaji huyo na kutafuta aliyebora zaidi, lakini wanasubiri na kujiridhisha kama ataweza kubadilika katika kipindi klichosalia kabla ya msimu huu haujafikia kikomo mwezi Mei.

Inaelezwa kuwa nahodha huyo wa Taifa Stars hajafikia matarajio ya kocha wa timu hiyo, Erol Bulut aliyokuwa anatarajia kutoka kwake, hasa baada ya kumfuatilia akiwa KRC Genk, kabla ya kutua Aston Villa.

Samatta, ambaye alitua Villa Park kwa ada ya uhamisho wa Pauni 8.5milion akitokea Ubelgiji ambako alikuwa akiichezea KRC Genk, Januari 2020, alijiunga na Fenerbahce kwa mkopo wa msimu mzima, mwezi Septemba mwaka jana, na kisa alisajiliwa moja kwa moja.

Akiwa na uzi timu hiyo kwenye mchezo wake wa kwanza kutupia, nahodha huyo wa Taifa Stars alifunga mabao mawili, ambapo ilikuwa mwanzoni mwa Oktoba, 2020 na ilikuwa mchezo wa Ligi dhidi ya Fatih Karagumruk. Walishinda kwa mabao 2-1.

Tangu hapo Samatta ameishia kufunga mabao mengine mawili ndani ya michezo 17 aliyocheza ya Ligi ambapo ilikuwa dhidi ya Ankaragucu na Kayserispor.

Samia afungua Mkutano wa Kimataifa wa uwekezaji
Namungo FC yapangwa na Waarabu