Uongozi wa klabu ya Fenerbahce ya nchini Uturuki, imeonyesha kutoshtushwa na majeraha ya jicho yanayomkabili mshambuliaji wa zamani wa Arsenal na Manchester United Robin van Persie.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 33, alifunga bao la kuongoza katika mchezo wa ligi uliochezwa jana dhidi ya Akhisar ambao walikubali kufungwa mabao matatu kwa moja.

Katika dakika ya 37 Van Parsie alishindwa kuendelea na mchezo baada ya kupata jeraha la jicho na kulazimika kutolewa nje ya uwanja kwa usaidizi wa watu wa huduma ya kwanza, baada ya kugongana na mchezji wa timu pinzani.

Image result for Fenerbahce play down fears over eye injury to Robin van PersieRobin van Persie alipogongana na mchezaji wa Akhisar 

Picha za televisheni zilionyesha tukio la kuumia kwa mshambuliaji huyo kutoka nchini Uholanzi, zilionyesha aliumia na kutokwa na damu katika sehemu ya jicho la upande wa kushoto, lakini dakika chache baada ya mchezo kumalizika uongozi wa Fenerbahce ulitoa taarifa njema kwa mashabiki ambazo zilieleza Van Parsie anaendelea vizuri.

“Alipatwa na tatizo la jicho lakini kwa uchunguzi wa awali imeonekana sio kubwa sana,” ilieleza taarifa ilitotolewa na daktari Burak Kunduracıogl.

“Tumejiridhisha jeraha lake halitomuweka nje kwa muda mrefu, lakini kwa siku kadhaa atakua katika uangalizi wa kimatibabu.

Takukuru yazipekua tuhuma za rushwa ya Milioni 10 kwa wabunge wa CCM
Jack Wilshere Arejeshwa Kundini