Mlinzi wa kati wa zamani wa Manchester United, Rio Ferdinand anatarajia kutangaza kuingia rasmi katika mchezo wa masumbwi licha ya kuwa na umri wa miaka 38.

Ferdinand amekuwa akiweka video kwenye mitandao ya kijamii zinazo muonyesha akifanya mazoezi ya masumbwi na alioneka katika uwanja wa Wembley mapema mwezi Aprili akishuhudia pambano la uzito wa juu kati ya bondia wa Uingereza Anthony Joshua na Wladimir Klitschko.

Wacheza soka wengine waliohamia katika masumbwi ni pamoja na Leon McKenzie na kiungo wa zamani wa klabu ya Birmingham Curtis Woodhouse aliyeshinda ubingwa wa British super lightweight mwaka 2014.

Mchezaji huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza anatarajia kufanya mkutano na waandishi wa habari leo kutangaza rasmi kuingia katika masumbwi.

Kwa sasa Ferdinand aliyezichezea klabu za West Ham United, Bournemouth, Leeds United, Manchester United na Queens Park Rangers amestaafu kucheza soka na ni mchambuzi wa soka katika kituo cha televisheni cha BtSport.

Rais Dkt. Shein aanza kupanga mikakati ya ushindi 2020
Urusi, Marekani kutatua mzozo wa Syria