Aliyekua meneja wa klabu ya Man Utd, Sir Alex Ferguson amewapasha habari mashabiki wa klabu ya Man City, kwa kuwaambia wasahau kuona mabadiliko ya klabu yao kutoka ilipo sasa na kufikia mafanikio ya FC Barcelona, kwa kisingizo cha ujio wa meneja kutoka nchini Hispania, Pep Guardiola.

Ferguson, amesema utakua upuuzi kwa kila shabiki kuamini hivyo, kutokana na falsafa za klabu ya Man city kutoshabihiana hata kidogo na klabu ya Barcelona, ambayo iliwahi kunolewa na Guardiola ambaye atajiunga nao mwishoni mwa msimu huu.

Babu huyo aliyestaafu kufundisha soka akiwa na heshima kubwa duniani kote, amesema Guardiola atakwenda Man city akiwa na malengo la kuiwezesha klabu hiyo kutwaa mataji, nasi kuifanya kufikia hatua kama ilivyo FC Barcelona kwa sasa.

Hata hivyo amedai kwamba pamoja na mipango hiyo ya meneja huyo, bado atakabiliwa na changamoto kubwa ya ushindani unaendelea kukua katika soka nchini England, hivyo amemtaka mspaniola huyo kujiandaa na hilo huku akiwasisitiza mashabiki kukubaliana na hali halisi itakayojitokeza.

“Man City ni klabu ambayo ina mipango tofauti na katu huwezi kuifananisha na FC Barcelona, hivyo ujio wa Guardiola hauwezi kukufanya utambe na kuamini mnakwenda kuwa bora kuliko wengine katika soka la England.” Amesema Ferguson.

“Kila meneja anayekuja hapa huwa na malengo yake ya kupambana lakini changamoto anazokutananazo huwa zinaonekana hadharani, hivyo kwa Pep litakua wazi na kila mmoja wetu anasubiri kuona hivyo.” Aliongeza Ferguson

Katika hatua nyingine babu huyo mwenye umri wa miaka 74, amesema ushindani wa soka la nchini England daima utaendelea kusalia katika klabu nguli kama Man Utd, Arsenal, Liverpool, Chelsea, Man City na Tottenham hata ikitokea malaika anashushwa kutoka mbinguni.

Amedai kwamba ni vugumu kufanya mapinduzi ya ushindani katika klabu hizo ambazo kila msimu zimekua zikileta changamoto kubwa dhidi ya klabu nyingine, hivyo hata kwa Pep bado anaamini atakubaliana na alichokisema hii leo.

“Pep atafanikiwa kuleta mabadiliko Man city kwa mbinu tofauti, lakini umwamba wa klabu za Man City, Arsenal, Liverpool, Chelsea na Tottenham utaendelea kubaki kama ilivyokua miaka ya nyuma hadi hivi sasa.” Ferguson alisisitiuza.

Pep Guardiola amekua gumzo tangu alipotangaza kutaka kuhamia nchini England mara tu mkataba wake utakapomalizika FC Bayern Munich na sasa imekua zaidi ya habari kutokana na mikakati aliyoanza kuifanya akiwa nje ya Man City kwa kuangalia nani atakaemfaa wakati wa kipindi cha usajili wa wachezaji.

Kamishna Mkuu wa Zamani wa TRA, Miss Tanzania wafikishwa mahakamani kwa ufisadi
Picha Ya Timu Ya Taifa Ya Ujerumani Yazua Tafrani