Swansea City wamekubalia kumsajili mshambuliaji kutoka nchini Hispania na klabu ya Sevilla CF, Fernando Llorente.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 31, anatarajiwa kuelekea Liberty Stadium mjini Swansea hii leo, kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya, kabla ya kukamilisha dili la kujiunga na klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini England.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa, mshambuliaji huyo ambaye aliwahi kuzitumikia klabu za Athletic Bilbao ya Hispania pamoja na Juventus FC ya Italia, atasaini mkataba wa miaka miwili na wa kuitumikia Swansea city.

Llorente anaelekea katika ligi ya nchini England, huku akijivunia mafanikio aliyowahi kuyapata katika ligi ya nchini Italia (Sirie A) ambapo alitwaa ubingwa mara tatu akiwa na Juventus FC pamoja na kucheza mchezo wa hatua ya fainali wa ligi ya mabingwa barani Ulaya mwaka 2015.

Mbali na mafanikio hayo, pia Llorente alikuwa sehemu ya kikosi cha Hispania kilichotwaa ubingwa wa dunia mwaka 2010 pamoja na kwenye fainali za mataifa ya barani Ulaya za mwaka 2012.

Luis Suarez: Daima Nitaipenda Na Kuithamini Liverpool
Mke wa Lissu afunguka ya baada ya kumsikia mumewe akilia 'njaa' kituo cha Polisi