Mbunge Jimbo la Makete kwa tiketi ya CCM Festo Richard Sanga, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, baada ya maombi yake kukubaliwa na kuingizwa kwenye Bajeti ya mwaka wa fedha 2021/22 iliyosomwa juma lililopita Bungeni, mjini Dodoma.

Sanga ambaye aliwahi kuwa Mkurugenzi wa klabu ya Singida United FC, ametoa shukurani hizo kwa kuandika waraka mzito na kuusambaza kwenye mitandao ya kijamii.

Waraka wa mdau huyo wa michezo nchini, umeanza na kichwa cha habari kisemacho: NIMESIMAMA BUNGENI KUISHUKURU SERIKALI (MH RAIS “MAMA YETU” SAMIA SULUHU HASSAN)

Leo tar 17/06/2021 nimesimama Bungeni kutoa shukrani za dhati kwa Bajeti iliyoletwa na serikali ikiwa imejumuisha mambo matatu (3) niliyoishauri serikali na mawili (2) niliyomuomba Mh Rais na ametolea maelekezo hasa kuhusu sekta ya Michezo nchini kama ifuatavyo.

1.Niliiomba na kuishauri serikali kuondoa kodi kwenye nyasi bandia ili kuwezesha viwanja vingi kuwekwa nyasi hizo na mpira wa Nchi yetu ukachezwa katika maeno safi na yenye hadhi ya soka. MAMA YETU kupitia Bajeti kuu ya serikali amekubali ombi hilo (Nyasi hizo ziwe kwa nchi nzima na sio Majiji tu, BMT wapewe kazi ya kucontro-Kutoa vibali kwa waagizaji).

2.Niliiomba na kuishauri serikali,Makapuni ya BETTING nchini yachangie michezo hasa mpira wa Miguu, “MAMA YETU” kupitia Bajeti kuu ya serikali amekubali Ombi hilo na sasa 5% itakuwa inapelekwa kwenye michezo.

3.Niliiomba na kuishauri serikali kuchukua hatua dhidi ya faini kubwa kwa Bodaboda kiasi ambacho kinakwamisha sana shughuli zao, “MAMA YETU” kupitia Bajeti ya serikali Kuu amekubali Ombi hilo, sasa Bodaboda faini ni 10,000 toka 30,000 ya Mwanzo.

4.Niliiomba na Kuishauri serikali kujenga Academy za Soka Nchini kikanda kama inawezekana, “MAMA YETU” amekubali Ombi hilo na amelitolea maelekezo kwa wizara husika kuanza mchakato wa kujenga Academy kila Mkoa.

5.Niliomba na kuishauri serikali kufanya mazungumzo na CCM ambao ni Wamiliki wa Viwanja  bya soka vingi nchini, Viwanja hivi viboreshwe na kama imeshindikana wapewe wawekezaji waviendeleze kwa makubaliano maalum. “MAMA YETU” amesiki Kilio hili na ametoa maelekezo CCM kuweka Nyasi bandia viwanja vyote na kama watashindwa wampatie muwekezaji ili viwanja viwe na ubora wa kutumika.

Mama kaupiga Mwingi sana sanaaa.

Festo Richard Sanga

Mbunge-Makete

17/06/201

Mkataba kuandaa mitaala ya shule za ufundi kusainiwa
Eriksen kupandikizwa betri kifuani