Nguli wa Hip Hop, Fareed Kubanda aka Fid Q ametangaza mpango wake wa kutoa kitabu kinachozungumzia maisha yake.

Ngosha ameweka wazi mpango huo kupitia Twitter baada ya kupewa pongezi na mbunge wa Bumbuli, January Makamba pamoja na Maria Sarungi kwa kazi nzuri aliyoifanya kwenye wimbo ‘Sheri’ alioshirikishwa na Rich Mavoko.

Amesema kitabu hicho kinaitwa ‘The Swahili Kid’ ambacho kitaambatana na albam yake ya tatu ‘Kitaaolojia’ ambayo amekuwa akiihubiri kwa muda mrefu.

Mashabiki wa rapa huyo wamekuwa wakiisubiri ‘Kitaaolojia’ kwa muda mrefu, albam ambayo inatarajiwa kuzungumzia maisha ya mtaani na hasa yanayomgusa moja kwa moja.

Huenda albam hiyo ikawa moto wa kuotoa mbali kwa kuzingatia kauli aliyowahi kuitoa mtayarishaji nguli wa muziki wa kizazi kipya, P-Funk Majani kuwa rapa huyo kwake ndiye rapa bora duniani.

Majani alieleza kuwa amempa nyota hizo Ngosha kwani kila anapoingia studio hufanya maajabu.

Agosti 13 mwaka huu, alipokuwa akiadhimisha siku yake ya kuzaliwa, Ngosha aliachia nyimbo mbili kwa mpigo alizozibatiza majina ya ‘Fresh’ na ‘Ulimi Mbili’.

Mourinho akoshwa na kiwango cha Matrial
Mwanachuo akamatwa kwa kumiliki bastola