Mwanamapinduzi wa Cuba, Fidel Alejandro Castro jana alitoka hadharani na kutoa hotuba yake kwa viongozi wa chama chake cha ‘Kikomunisti’ alichokiweka madarakani zaidi ya miaka 50 iliyopita huku akijitabiria kifo.

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 89 aliwaambia viongozi hao kuwa ana muda mfupi atafariki kwakuwa anafikisha umri wa miaka 90 hivi karibu. Lakini aliwataka viongozi hao kuhakikisha haiutupi wala kuuacha ‘ukomunist’.

“Nitakuwa na umri wa miaka 90 hivi punde,” alisema Castro. “Hivi punde nitakuwa kama wale wengine [nitakufa]. Muda utafika kwetu wote, lakini mawazo ya wakomunisti wa Cuba itabaki kama uthibitisho kwenye hii sayari kwamba kama tutafanya kwa kazi hisia zote na heshima, tunaweza kuzalisha vifaa na bidhaa za kitamaduni ambazo binadamu wanahitaji, na tunapaswa kupambana bila hasira za kuwafikia,” alieleza.

Alitoa hotuba hiyo ikiwa ni siku chache baada ya serikali kutangaza kuwa kaka yake Raul Castrol atachukua nafasi ya juu zaidi ya chama cha Kikomunisti.

Fidel Castro amekuwa Rais wa Cuba tangu mwaka 1976 hadi mwaka 2008 kabla hajamuachia nafasi hiyo kaka yake Raul.

 

Yanga yajipanga kuumana na Al Ahly, Mtihani wenye majibu yaliyojificha
Madini ya Mabilioni yaliyonaswa yakitoroshwa kukabidhiwa Rasmi kwa tajiri mwenye ubavu