Shirikisho la soka duniani FIFA limeanza kufanya uchunguzi wa kitendo cha timu za taifa za England na Scotland kuvaa vitambaa vyeusi vilivyokua na lebo nyekundu ambayo inaashiria kumbukumbu ya mashujaa wa nchi hizo waliopoteza maisha katika vita ya kwanza ya dunia.

Kamati ya nidhamu ya FIFA, imekabidhiwa jukumu hilo, na wakati wowote itakapobainika sababu za timu hizo kuvaa nembo hiyo itatangaza maamuzi yatakayochukuliwa.

FIFA imekua ikipinga masuala ya kisiasa kuchanganywa kwenye mchezo wa soka, kwa kuhofia vurugu za kiitikadi ambazo huenda zikajitokeza miongoni mwa wanafamilia wa mchezo huo.

Hata hivyo klabu za ligi zote za nchini Scotland na England zimekua zikivaa lebo nyekundu katika mavazi yao, na miaka yote imekua ikifanyika kila inapofika mwezi Novemba.

Katika mchezo huo wa kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia za mwaka 2018, England walifanikiwa kuchomoza na ushindi wa mabao matatu kwa sifuri.

Lionel Messi Apinga Agizo La Benchi La Ufundi FC Barcelona
Video: Mrema alia na jeshi la magereza