Shirikisho la soka duniani FIFA, limebariki adhabu iliyotolewa na kamati ya maadili, dhidi ya watuhumiwa wa ubadhilifu wa fedha, rais Sepp Blatter pamoja na rais wa UEFA, Michel Platini.

Wawili hao wamefungiwa kwa kipindi hicho, ili kupisha uchunguzi uliodhamiriwa kufanywa na serikali ya nchini Usiwiz.

Adhabu kama hiyo pia imemkuta aliyekua katibu mkuu wa FIFA, Jerome Valcke, ambaye tayari alikua ameshawekwa pembeni kutokana na tuhuma hizo.

                                                              Jerome Valcke

Naye  Chung Mong-joon ambaye alikua makamu wa rais wa FIFA, ameadhibiwa kwa kufungiwa miaka sita, sambamba na kutozwa faini ya Franga za Uswiz 100,000.

                                                          Chung Mong-joon 

Watuhumiwa hao wamekubwa na adhabu hizo, kutokana na malipo hewa ya paund million 1.35, yanayodaiwa kufanywa, kwa kuhusushwa viongozi hao, huku wakijua ni kosa kubwa kujiingiza kwenye ufusadi.

Kutokana na maamuzi hayo FIFA umemteua raisi wa shirikisho la soka barani Afrika CAF, Issa Hayatou, kukaimu nafasi ya urais mpaka uchaguzi wa rais utakapofanyika februari 26 mwaka 2016.

Mbeya City Wachimba Mkwara
Gus Poyet Domínguez Ampigia Pande Sam Allardyce