Shirikisho la soka duniani FIFA, kupitia kamati yake ya maadili, imethibitisha kuanza kumfanya uchunguzi wa kina dhidi ya gwiji wa soka kutoka nchini Ujerumani, Franz Beckenbauer ambaye anatajwa kuwa sehemu ya wanaojihusisha na masuala la ufisadi.

Uchungzi huo, pia utamuhusu mwenyekiti wa chama cha soka nchini Hispania Angel Maria Villar Llona, ambaye anatajwa kuwa na mahusiano ya kifisadi la viongozi wa juu ambao wameshasimamishwa na kamati hiyo kwa siku 90 Sepp Blatter pamoja na Michel Platini.

Wawili hao wameingia kwenye uchunguzi, kutokana na kukataa kutoa ushirikiano dhidi ya timu inayoendelea kusaka ukweli wa jambo la kifisadi linalotajwa kufanywa na viongozi wa juu kwa kulipana fedha kinyume na taratibu.

Beckenbauer, pamoja na Villar, ambao ni sehemu ya wajumbe wa kamati ya utendaji ya FIFA, wamefikia hatua ya kufuatiliwa kwa ukaribu, kutokana na kusemekana walihusika kwenye mchakato wa kutoa nafasi kwa wenyeji wa fainali za kombe la dunia za mwaka 2018 pamoja na 2022.

Beckenbauer, mwenye umri wa miaka 68, pia anatajwa kuhusika na masuala la mlungula ambayo yalidaiwa kuchukua nafasi wakati nchi ya Ujerumani ilipofanikiwa kuwa mwenyeji wa fainali za kombe la dunia za mwaka 2006.

Kwa upande wa Villar, ambaye amekua mwenyekiti wa chama cha soka nchini Hispania tangu mwaka 1988, anatajwa kuwa mtu wa karibu sana na rais wa UEFA Michel Platini, hali ambayo imezua hofu kubwa ya kuwepo kwa harufu ya kushirikiana katika masuala ya kukiuka maadili.

Villar, anatajwa kuwa mshawishi ndani ya UEFA, kwa kuipa kipaumbele nchi yake ya Hispania pamoja na Ureno ili ziwe sehemu ya wenyeji wa fainali za kombe la barani Ulaya za mwaka 2018, lakini hata hivyo hatua hiyo ilishindikana, baada ya  nchi ya Urusi kushinda kinyang’anyiro hicho.

Pellegrini: De Bruyne Ametupa Heshima
Chadema wataja asilimia za ‘ushindi wa Lowassa’